POPULAR FOLLOW IN wORLD WITH 444 KG: MTU MWENYE UNENE MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI AFARIKI DUNIA...ALIKUWA NA KILO 444!
Leo
kuna taarifa kuhusu mtu aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mnene
kuliko wote duniani kwa kuwa na uzito wa Kilo 444, Keith Martin ambaye
amefariki akiwa na umri wa miaka 44.
Wakati
wa uhai wake aliwahi kufanywa upasuaji na robo tatu ya nyama za kwenye
tumbo lake ilikuwa imeondolewa na kufanikiwa kumpunguza nusu ya uzito wa
mwili wake, ambapo kifo chake kimetokea miezi nane toka afanyiwe
upasuaji huo kwa kuugua ugonjwa wa Pneumonia.
Kabla
ya upasuaji Martin alikuwa anakula Calories 20,000 kiasi ambacho ni
mara kumi ya kiasi ambacho kinapendekezwa kuliwa na mtu mzima.
Moja
ya vitu alivyopendelea kula wakati wa kifungua kinywa ni Pizza na Mayai
na kutokana na tatizo la uzito mkubwa Martin aliwahi kukaa ndani ya
nyumba yake huko Uingereza kwa miaka 10 bila kutoka nje kutokana na
kuelemewa na uzito mkubwa.
Moja ya dada zake amesema wana majonzi kumpoteza ndugu yao na bado wanaendelea kuomboleza msiba huo.
POPULAR FOLLOW IN wORLD WITH 444 KG: MTU MWENYE UNENE MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI AFARIKI DUNIA...ALIKUWA NA KILO 444!
Reviewed by ibigezwehobyose
on
Saturday, July 04, 2015
Rating: