Mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Mwandishi wetu
DAKTARI
wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Dokta
Fadhili Emily, amemnunulia baiskeli ya kubebea mtoto, mpenzi wa Nasibu
Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kama zawadi pindi
atakapojifungua.
Mfano
wa baiskeli aliyitoa Dkt. Fadhili kwa Zari. Akizungumza na Risasi
Mchanganyiko akiwa nchini Sweden alikoenda kwa ziara binafsi, Dokta
Fadhili alisema kwa kutambua yeye ni mtu wa Kigoma anakotokea Diamond,
ameona amnunulie shemeji yake huyo baiskeli hiyo ambayo kwa mujibu wake,
ina thamani ya shilingi milioni 5 za Kitanzania.
Dkt.
Fadhili Emily. “Mimi ni mwenyeji wa Kigoma, Zari ni shemeji yangu hivyo
nikiwa huku Sweden nimeona niwawakilishe vijana wote wa kule kwa
kumnunulia baiskeli hii ya kisasa shemeji yetu, wanatumia wanawake wengi
Ulaya kubebea watoto wao,” alisema.
Zari anatarajiwa kujifungua kati ya Agosti au Septemba, mwaka huu ambapo ujio wa mtoto huyo umekuwa ukitengeneza vichwa vya habari kila kukicha.
Zari anatarajiwa kujifungua kati ya Agosti au Septemba, mwaka huu ambapo ujio wa mtoto huyo umekuwa ukitengeneza vichwa vya habari kila kukicha.
ZARI aka Lady Boss APEWA ZAWADI YA BAISKELI YA MILIONI 5
Reviewed by ibigezwehobyose
on
Wednesday, June 24, 2015
Rating: